• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Masumbwi, Uzito wa Juu: Bondia Dillian Whyte amshinda Joseph Paker

    (GMT+08:00) 2018-07-30 11:11:05

    Katika pambano la raundi 12 lililosubiriwa kwa muda mrefu na mashabiki wa masumbwi kote duniani na kufanyika mjini Cardiff nchini Wales, bondia Dillian Whyte wa Uingereza alifanikiwa kupata ushindi kwa njia ya pointi dhidi ya mpinzani wake Joseph Parker wa New Zealand.

    Whyte alishinda kwa wingi wa pointi, kulingana na majaji akipata 113-112, 115-110, 114-111, na bondia huyo kwa sasa anatazamiwa kuanza maandalizi ya kuwania mikanda ya uzito wa juu dhidi ya Deontay Wilder wa Marekani au Anthony Joshua wa Uingereza.

    Kwa upande wa mapambano ya Utangulizi, mwanadada Katie Taylor kutoka Ireland ya Kaskazini alimshinda Kimberley Connor wa Marekani kwa KO katika raundi ya tatu, na bondia huyo sasa amefanikiwa kutetea mataji yake ya ubingwa wa IBF na WBA.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako