• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Israel lashikilia meli ya msaada wa kimataifa inayoelekea kanda ya Gaza

    (GMT+08:00) 2018-07-30 16:23:49

    Jeshi la majini la Israel jana lilizuia meli ya msaada wa kimataifa iliyotoka Ulaya na kuelekea Ukanda wa Gaza.

    Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Israel imesema, meli hiyo ilijaribu kuvunja kizuizi halali cha baharini kilichowekwa na Israel dhidi ya Ukanda ya Gaza,hivyo jeshi la majini limeishikilia meli hiyo kwa kufuata sheria ya kimataifa.

    Jeshi hilo pia limesema, kabla ya kuizuia meli hiyo, abiria wake waliarifiwa kukiuka kizuizi halali cha baharini, na kuongeza kuwa vifaa vya msaada wa binadamu vinaweza kupitia bandari ya Ashdod, kusini mwa Israel na kupelekwa Ukanda wa Gaza.

    Hivi sasa meli hiyo imehamishwa kwa bandari ya Ashdod na hakuna madhara yaliyotokea katika mchakato wa kuizuia meli hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako