• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uingereza yapenda kushirikiana na China kulinda biashara huria na utaratibu wa pande nyingi

    (GMT+08:00) 2018-07-30 17:14:39

    Balozi wa Uingereza nchini China Bi. Barbara Janet Woodward amesema, ikiwa mlinzi wa utaratibu wa pande nyingi, Uingereza inapenda kushirikiana na China kulinda utaratibu huo na kuhimiza biashara huria.

    Bi. Woodward amesema, Uingereza inaipongeza China kwa kuendelea na hatua za kufungua mlango zaidi, na itatuma ujumbe wa ngazi ya juu kushiriki kwenye maonesho ya kimataifa ya kwanza ya bidhaa zinazoagizwa kutoka nje nchini China yatakayofanyika mwezi Novemba mjini Shanghai mwaka huu.

    Wakati huo huo, Bi. Woodward amesema, serikali ya Uingereza ina msimamo ulio wazi kwa uwekezaji kutoka China, akiongeza kuwa Uingereza ni moja ya nchi zinazovutia uwekezaji kwa wingi zaidi barani Ulaya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako