• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mazungumzo ya tisa ya kimkakati kati ya China na Uingereza yafanyika

    (GMT+08:00) 2018-07-30 19:09:50

    Mjumbe wa taifa ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi na waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Bw. Jeremy Hunt wamefanya mazungumzo ya tisa ya kimkakati leo asubuhi hapa Beijing.

    Baada ya mazungumzo hayo mawaziri hao wawili walikutana na waandishi wa habari, ambapo Bw. Wang Yi alikuwa na haya ya kusema:

    "Bw. Hunt amekuja Beijing ndani ya mwezi mmoja tangu aliposhika wadhifa wa uwaziri wa mambo ya nje, na kufanya mazungumzo ya tisa kati ya China na Uingereza, hatua ambayo imeonesha ufuatiliaji mkubwa wa Uingereza katika kukuza uhusiano kati ya pande hizi mbili. Tumefikia makubaliano mengi kwenye mazungumzo hayo."

    Pia ameeleza kuwa China inatumaini kuwa Uingereza itajiunga na ushirikiano wa pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" kwa juhudi kubwa zaidi, na pia inawakaribisha viongozi wa Uingereza kuhudhuria Mkutano wa kilele wa pendekezo hilo utakaofanyika mwaka ujao.

    Bw. Hunt amesema, Uingereza inatumaini kuimarisha mazungumzo ya kimkakati kati yake na China, kukuza urafiki,na kuimarisha mawasiliano na ushirikiano katika nyanja mbalimbali, ili kukabiliana na changamoto mbalimbali, na kulinda uhusiano wa pande nyingi na utaratibu wa kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako