• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa UM atoa wito wa juhudi zaidi kutokomeza magendo ya binadamu

    (GMT+08:00) 2018-07-31 08:58:36

    Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Bw. Antonio Guterres ametoa wito wa juhudi zaidi kutokomeza magendo ya binadamu. Kwenye taarifa yake ya kuadhimisha Siku ya kimataifa ya kupambana na magendo ya binadamu, Bw. Guterres amesema magendo ya binadamu hufanyika kwa njia nyingi na kwa kuvuka mipaka ya nchi, lakini watendaji wa uhalifu huo huwa hawadhibitiwi ipasavyo, hali ambayo inatakiwa kubadilishwa.

    Amesema magendo ya binadamu ni uhalifu unaotokana na machafuko na kukosekana kwa usawa na utulivu, na watendaji wa uhalifu huo wanawalenga watu walio kwenye hatari haswa wanawake na watoto, na kuwanyima haki zao za kimsingi. Bw. Guterres amesema Umoja wa mataifa utachukua hatua madhubuti kuwafikisha wahalifu mbele ya sheria, na kuwalinda wahanga wa uhalifu huo, ambao ameutaja kama utumwa mamboleo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako