• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 11 wafariki katika ajali ya barabarani kusini magharibi mwa Uganda

    (GMT+08:00) 2018-07-31 08:59:14

    Polisi nchini Uganda wamesema watu 11 wamefariki dunia papo hapo na wengine 22 wamejeruhiwa baada ya lori walilokuwa wanasafiria kupinduka kwenye eneo la Kisoro, kusini magharibi mwa Uganda mapema jana.

    Naibu msemaji wa polisi Bw. Patrick Onyango amesema lori lililokuwa limebeba wafanyabiashara 30 na bidhaa zao, lilipinduka mara kadhaa baada ya kushindwa kukata kona kali kwenye barabara kati ya Kisoro na Rubanda, karibu na kijiji cha Kigowa.

    Kamanda wa polisi eneo la Kisoro Bw. Charles Okoto amesema dereva alitoroka baada ya kutokea kwa ajali hiyo, na kwamba inawezekana kuwa alikuwa anaendesha gari baada ya kunywa pombe.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako