• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasema umwamba wa kiuchumi haukubaliki na matishio na mashinkizo havitafanikiwa

    (GMT+08:00) 2018-07-31 09:02:33

    China na Uingereza zimeahidi kushirikiana na jumuiya ya kimataifa katika kulinda utaratibu wa pande nyingi, mfumo wa biashara huria na kanuni za Shirika la Biashara Duniani WTO.

    Ahadi hiyo imetolewa kwenye mazungumzo ya 9 ya kimkakati kati ya China na Uingereza yaliyofanyika kati ya waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi na mwenzake wa Uingereza Bw. Jeremy Hunt.

    Wakikutana na wanahabari baada ya mazungumzo, Bw. Wang amesema tangu mwanzoni mwa mwaka huu, China na Marekani zimefanya majadiliano mara kadhaa kuhusu suala la biashara, na pia zimefikia makubaliano mengi. Kinachosikitisha ni kuwa Marekani haifuati ahadi zake na haiendi sambamba na China. Bw. Wang amesisitiza kuwa mageuzi na ufunguaji mlango ni sera ya taifa ya China, na ni msimamo wazi wa China kwamba migogoro ya kibiashara inapaswa kutatuliwa kwa njia ya mazungumzo na wala sio mapambano.

    Bw. Wang ameongeza kuwa mlango wa China uko wazi kwa mazungumzo, lakini yanapaswa kufanywa kwenye msingi wa usawa na kuheshimiana. Amesisitiza kuwa sera ya upande mmoja. na umwamba wa kiuchumi havikubaliki kwa nchi yoyote, na matishio na mashinikizo ya upande mmoja havitafanikiwa na huleta matokeo kinyume na matarajio.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako