• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yatoa ardhi kwa balozi za nchi mbalimbali kuhamia kwenye mji mkuu mpya

    (GMT+08:00) 2018-07-31 09:14:53

    Rais John Magufuli wa Tanzania jana alitangaza kugawa ardhi kwa balozi za nchi mbalimbali na mashirika ya kimataifa kwa ajili ya ofisi na makazi yao kwenye mji mkuu wa nchi hiyo Dodoma.

    Rais Magufuli alikabidhi hati 62 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za ubalozi, na hati tano kwa ajili ya mashirika ya kimataifa yaliyoko Tanzania, ili kufanikisha kuhamia kwao mjini Dodoma.

    Baadhi ya balozi zilipokea hati hizo ni pamoja na Uingereza, Ubelgiji, Canada, Ufaransa na Kenya, na mashirika yaliyopokea hati hizo ni pamoja na Shirika la kazi dunia ILO, Umoja wa mataifa, Shirika la fedha Duniani IMF na benki ya maendeleo ya Afrika AfDB.

    Rais Magufuli amesema makamu wa Rais na Waziri mkuu tayari wamehamia Dodoma, na karibu mawaziri wote na maofisa waandamizi wa serikali wamehamia Dodoma. Yeye mwenyewe amesema anapanga kuhamia Dodoma kabla ya mwisho wa mwaka huu, na hataki kuwaacha mabalozi hao Dar es salaam.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako