• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iran yataja biashara ya mafuta kwa dhahabu na Afrika kuwa "ufumbuzi" wa vikwazo vya Marekani

    (GMT+08:00) 2018-07-31 09:31:17

    Ofisa wa biashara wa Iran amesema Iran inatafuta ufumbuzi mbadala wa kudumisha biashara na Afrika kwa njia ya kubadilishana mafuta kwa dhahabu.

    Mwenyekiti wa baraza la ushirikiano wa kiuchumi kati ya Iran na Afrika Bw Hassan Khosrowjerdi, amesema kutokana na vikwazo vitakavyowekwa na Marekani, suala la benki litakuwa changamoto kubwa inayoikabili Iran katika kufanya biashara na nchi niyingine.

    Amesema suala hilo linaweza kutatuliwa kwa kuweka mpango wa kubadilishana bidhaa na nchi nyingine, zikiwemo nchi za Afrika. Ameongeza mpango huo ni njia mwafaka ya kudumisha biashara na nchi za Afrika, hasa katika kipindi maalumu cha vikwazo.

    Wakati huo huo, rais Donald Trump wa Marekani amesema yuko tayari kukutana na mwenzake wa Iran Hassan Rouhani bila masharti yoyote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako