• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WFP na Ethiopia zahitaji fedha zaidi kuwasaidia wakimbizi

    (GMT+08:00) 2018-07-31 09:50:55

    Serikali ya Ethiopia na shirika la mpango wa chakula duniani wametoa wito wa fedha zaidi kutolewa kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya kibinadamu ya wakimbizi walioko nchini Ethiopia.

    Ethiopia na shirika hilo wametoa mwito huo wakati Ethiopia inafanya juhudi kubwa kutoa msaada wa kibinadamu kwa wakimbizi karibu milioni 1 kutoka Sudan Kusini, Somalia na Eritrea walioko nchini Ethiopia.

    Kwa mujibu wa mamlaka ya wakimbizi na mambo ya kuwarudisha nyumbani ya Ethiopia ARRA, changamoto nyingi zinazoikabili serikali ya Ethiopia katika kuwasaidia wakimbizi zinatokana na upungufu wa fedha na uungaji mkono.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako