• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China asisitiza kuimarisha mfumo kamili wa usimamizi wa chanjo

    (GMT+08:00) 2018-07-31 09:53:53

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang amesisitiza kuimarisha mfumo kamili wa usimamizi wa chanjo kwenye ngazi zote kote nchini.

    Bw. Li amesema hayo baada ya kusikiliza ripoti kutoka kwa timu ya uchunguzi ya baraza la mawaziri kuhusu chanjo bandia ya kichaa cha mbwa inayotumika kwa binadamu, iliyotengenezwa na kampuni ya kutengeneza chanjo ya Changsheng ya mji wa Changchun.

    Ripoti pia imeonesha vitendo vingi vya kampuni hiyo vya kukiuka sheria kama vile kubadilisha ovyo mchakato wa utengenezaji, kuweka rekodi ovyo za utengenezaji na ukaguzi, na kuvuruga ushahidi.

    Hivi sasa, polisi wameomba ruhusa ya kuwakamata watuhumiwa wa kesi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako