• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Soka, Ligi ya 8 bora Uganda: Mabingwa wa ligi Vipers SC wajitoa kwenye mashindano

  (GMT+08:00) 2018-07-31 10:18:12

  Shirikisho la mpira wa miguu la Uganda FUFA, limethibitisha kuwa mabingwa watetezi wa ligi kuu ya nchi hiyo Vipers SC hawatashiriki kwenye michuano maalum ya super 8 itakayofanyika kuanzia Agosti 4 mjini Kampala.

  Akitoa taarifa hiyo jana mjini Kampala mjumbe wa kamati kuu ya FUFA, Roger Byamukama, alisema kwa kuwa michuano hiyo inahusisha timu 6 bora za kutoka ligi kuu msimu uliopita, hivyo nafasi ya Vipers SC ambao wamejiondoa inachukuliwa na BUL ambao walimaliza katika nafasi ya saba msimu uliopita.

  Aidha kiongozi huyo amesema, michuano hiyo ambayo kwa mwaka huu ndiyo inafanyika kwa mara ya kwanza itakuwa ikifanyika kila mwaka ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako