• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Makocha na Waamuzi wa Triathlon wapewa mafunzo kuelekea michuano ya Rwanda

    (GMT+08:00) 2018-07-31 10:19:09

    Kuelekea mashindano ya kimataifa ya mbio mchanganyiko (Triathlon) mwezi ujao nchini Rwanda, shirikisho la Triathlon la Rwanda kwa kushirikiana na shirikisho la kimataifa, limeandaa semina maalum ya mafunzo kwa makocha wa mchezo huo ambao watatumika kusimamia uendeshaji wa michuano hiyo.

    Semina hiyo ya siku tano iliyoanza jana inaendeshwa na wakufunzi wa kimataifa, Laurent Massias kutoka chama cha Triathlon cha Ufaransa na kocha mkuu wa shirikisho la Triathlon la kimataifa Vicent Alcala kutoka Hispania na inahusisha washiriki 16 kutoka nchi za DRC, Burundi na Rwanda.

    Sambamba na semina hiyo, kutafanyika mafunzo kwa waamuzi watakaoongoza mashindano hayo ya siku moja yatakayofanyika Agosti 4 mjini Rubavu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako