• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kombe la Dunia 2022: Qatar yakana madai kuwa ilitumia rushwa

    (GMT+08:00) 2018-07-31 10:20:04

    Qatar imejitokeza na kupinga madai yote yaliyowasilishwa FIFA kuwa ilitumia rushwa ili kupata nafasi ya kuwa mwenyeji wa michuano ya kombe la dunia mwaka 2022.

    Qatar imefafanua hayo baada ya gazeti moja la nchini Uingereza kuitaka FIFA ifanye uchunguzi dhidi ya njia zilizotumika mwaka 2010 kuipatia nchi hiyo uenyeji wa michuano ya kombe la dunia mwaka 2022.

    Katika madai yaliyofikishwa FIFA, inasemekana kuwa Qatar ilitoa rushwa na kuunda kikosi-kazi kwa ajili ya kufanya njama za kuwafuta wapinzani wakati wa kinyang'anyiro cha kuwa wenyeji wa michuano ya kombe la dunia mwaka 2022.

    Wapinzani wa karibu wa Qatar kwa wakati huo walikuwa ni Marekani, Australia, Korea Kusini na Japan.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako