• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yasema "Ukanda Mmoja, Njia Moja" ni wazi na shirikishi, na unaongozwa na kanuni

  (GMT+08:00) 2018-07-31 10:47:42

  Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amesema China inakaribisha makampuni ya Uingereza katika huduma za fedha na sheria, na kushiriki kwenye miradi ya "Ukanda Mmoja, Njia Moja".

  Bw. Wang amesema hayo jana mjini Beijing alipokutana na waandishi wa habari baada ya mazungumzo ya 9 ya kimkakati kati ya China na Uingereza aliyoongoza pamoja na mwenzake wa Uingereza Bw. Jeremy Hunt. Amesema katika mazungumzo yao, wamejadiliana kwa kina kuhusu ushirikiano wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na pande hizo mbili zimekubaliana kuunganisha mikakati ya maendeleo, na kutafuta nguvu za ushirikiano ambazo hazijatumiwa ipasavyo katika sekta za fedha, sheria, uvumbuzi na ushirikiano na upande wa tatu.

  Bw. Wang amesisitiza kuwa pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" ni wazi na shirikishi, na China inakaribisha nchi zote kushiriki katika pendekezo hilo kama zinakubali mtazamo wa kushauriana kwa pamoja, kujenga kwa pamoja na kunufaika kwa pamoja. Pia amesema "Ukanda Mmoja, Njia Moja" unaongozwa na kanuni na sheria zinazotumiwa kimataifa, na China inatarajia pande mbalimbali zitafanya ushirikiano endelevu wenye vigezo vya juu, ubora wa hali ya juu na kutochafua mazingira.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako