• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China haina haja ya kudhibiti kiwango cha ubadilishaji wa sarafu yake RMB

    (GMT+08:00) 2018-07-31 10:48:04

    Marekani hivi karibuni imeishutumu China kudhibiti kiwango cha ubadilishaji wa sarafu yake ya RMB. Mchumi mkuu wa Shirika la Fedha Duniani IMF Bw. Maurice Obstfeld amesema hakuna ushahidi unaoweza kuthibitisha shutuma hiyo.

    "China kudhibiti kiwango cha ubadilishaji wa sarafu ya RMB" ni kisingizio kinachotumiwa na Marekani mara kwa mara. Ukweli ni kwamba kiwango hicho kinaamuliwa na soko, na China haipendi kuhamasisha mauzo ya bidhaa kwa kupunguza kiwango hicho. Wachambuzi wamesema hali hii inatokana na sababu tatu: kwanza, manunuzi ya ndani yamekuwa injini ya maendeleo ya uchumi wa China. Takwimu zinaonesha kuwa katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, manunuzi ya ndani yamechangia asilimia 78.5 ya ongezeko la pato la ndani GDP la China. Pili, sera ya kufungua mlango zaidi ni msingi imara wa thamani ya sarafu ya RMB. Tatu, kupunguza kiwango hicho hakutaleta faida kwa uchumi wa China, kwani China inajitahidi kuongeza oda ya bidhaa kutoka nje.

    Wachambuzi wanaona sababu halisi ya kupungua kwa kiwango cha sarafu ya RMB ni vita ya biashara iliyoanzishwa na Marekani, kupanda kwa kiwango cha ubadilishaji wa sarafu ya dola za kimarekani na kitendo cha Benki kuu ya Marekani cha kuongeza kiwango cha riba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako