• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Balozi wa China asema hakuna mwenye mamlaka ya kuzuia uhusiano wa China na Marekani

    (GMT+08:00) 2018-07-31 16:41:49

    Balozi wa China nchini Marekani Cui Tiankai amesema, ushirikiano ndio njia pekee sahihi kwa China na Marekani, kwa kuwa maslahi ya pamoja ya nchi hizo mbili ni makubwa kuliko tofauti zao.

    Akizungumza kwenye hafla ya kusherehekea miaka 91 ya kuanzishwa kwa Jeshi la Ukombozi la Watu wa China, balozi Cui amesema maslahi yaliyowekwa na watu wa nchi hizo mbili ni wajibu wa kihistoria wa kuweka sawa uhusiano wa China na Marekani, na sio huru kwa mtu yeyote kuuharibu.

    Amesema ni kawaida kwa nchi hizo mbili kuwa na ushindani katika baadhi ya maeneo, lakini ufunguo ni kwamba, ushindani kati yao unapaswa kuwa chanya, ukilenga kuboresha nchi zote mbili, na sio moja kuchukua nafasi ya nchi nyingine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako