• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa atoa wito kupambana na uhalifu wa biashara ya binadamu

    (GMT+08:00) 2018-07-31 16:59:59

    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ametoa wito kwa nchi zote kushikamana katika kupambana na biashara haramu ya binadamu.

    Bw. Guterres amesema hayo jana katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupinga biashara haramu ya Binadamu. Amesema usawa, utulivu wa kijamii na mapigano ya kutumia silaha ni chanzo cha biashara haramu ya binadamu, na wahalifu huwalenga watoto, vijana, wahamiaji na wakimbizi, na kuwanyima haki zao za msingi. Ameongeza kuwa, Umoja wa Mataifa unajikita kuwalinda na kuunga mkono waathirika, pia unawatafuta na kuwakamata wahalifu. Bw. Guterres ametoa wito kutilia maanani kukinga, kulinda na kuwajibika, ili kuzuia uhalifu wa biashara haramu ya binadamu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako