• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China azitaka China na Uingereza zishirikiane kulinda uchumi wa dunia ulio wazi

    (GMT+08:00) 2018-07-31 17:12:41

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang jana alasiri hapa Beijing amekutana na waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Bw. Jeremy Hunt ambaye yuko ziarani nchini China.

    Bw. Li amesema, zikiwa nchi wajumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na makundi muhimu ya kiuchumi duniani, China na Uingereza zina jukumu la kulinda utaratibu na mfumo wa kimataifa kwa msingi wa nia na kanuni za katiba ya Umoja wa Mataifa na utaratibu wa biashara ya pande nyingi kwa msingi wa Shirika la Biashara Duniani WTO. Amesema China na Uingereza zinatakiwa kushirikiana kulinda uchumi wa dunia ulio wazi, na kutilia nguvu ya kiujenzi yenye utulivu kwa dunia.

    Bw. Hunt amesema nchi hizo mbili zinapaswa kuimarisha mawasiliano na uratibu, kushikilia mfumo wa pande nyingi na biashara huria kwa pamoja, na kulinda utaratibu wa kimataifa kwa msingi wa kanuni husika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako