• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Utafiti waonesha kuwa asilimia 92 ya wahojiwa wana wasiwasi kuhusu usalama wa habari

    (GMT+08:00) 2018-07-31 17:15:37

    Gazeti la China Youth Daily limesema, kwa mujibu wa utafiti mpya, asilimia 92 ya watu wana wasiwasi kuhusu usalama wa taarifa zao binafsi.

    Asilimia 84.5 wamesema, wametakiwa kutoa taarifa zao binafsi kwa kampuni wakati wakipakua app za simu za mkononi huku asilimia 67 wakiamini kuwa watengenezaji wa app hizo wanaweza kupata kiholela habari za watumiaji.

    Zaidi ya asilimia 80 ya watu waliohojiwa wamesema, wamepata ujumbe usiotakiwa baada ya kujiandikishwa kwenye majukwaa fulani.

    Mchambuzi Bw. Xiong Ran amesema, baadhi ya watoaji wa huduma na majukwaa wameshindwa kufuata makubaliano ya kulinda taarifa binafsi za watu na kuuza taarifa hizo kwa watu wengine, wakati baadhi ya watumiaji wakipuuza njia za kulinda habari zao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako