• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwezi Julai kielelezo cha PMI katika viwanda vya utengenezaji nchini China chadumisha kiwango cha juu

    (GMT+08:00) 2018-07-31 17:19:55

    Idara ya takwimu ya China imetangaza kuwa, mwezi Julai kielelezo cha wasimamizi wa manunuzi PMI cha China kimefikia asilimia 51.2, kiasi ambacho kiko kwenye kiwango cha ukuaji. Wataalamu wanaona katika nusu ya pili ya mwaka huu, mwelekeo wa PMI utadumishwa kwenye kiwango hicho nchini China.

    Kielelezo cha PMI kinahusisha hatua mbalimbali za viwanda zikiwemo manunuzi, utengenezaji na uuzaji, ambacho kinachotumiwa zaidi duniani katika kusimamia mwelekeo wa jumla wa uchumi, na asilimia 50 ni kiwango cha katikati. Mtafiti kutoka kituo cha utafiti kuhusu maendeleo cha Baraza la serikali la China Bw. Zhang Liqun anasema:

    "Mwei Julai kiwango cha uzalishaji cha viwanda kimepungua kwa kiasi, hali hii inawezekana kusababishwa na mabadiliko ya misimu. Aidha kiasi cha oda mpya za uagizaji wa bidhaa nchini pia imepungua kiasi. Lakini kutokana na hali ya jumla, mwelekeo la ongezeko la uchumi haujabadilika, lakini chanzo cha upunguaji huo kinatakiwa kufuatiliwa."

    Bw. Zhao Liqun akizungumzia athari zinazoletwa na mikwaruzano ya biashara ya kimataifa kwa uchumi wa China, amesema uchumi wa China unategemea zaidi mahitaji ya soko la ndani, mabadiliko ya muundo kwa upande mmoja hayataathari vibaya hali ya jumla ya uchumi nchini China.

    Akizungumzia mwelekeo wa kielelezo cha PMI katika nusu ya pili ya mwaka huu, Bw. Zhang Liqun anasema:

    "Katika nusu ya pili ya mwaka huu, kutokana na hatua mbalimbali za fedha za kuchochea ukuaji wa uchumi zilizotangazwa na baraza la serikali la China, matatizo mbalimbali ikiwemo ukosefu wa fedha katika ujenzi wa miundo mbinu yatapungua kwa kiasi kikubwa. Wakati huo huo mahitaji ya soko la ndani yataongezeka, huku kiwango cha uwekezaji kikiinuka. Hivyo kielezo cha PMI kitadumishwa katika kiwango mwafaka."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako