• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Zimbabwe asema taarifa kuhusu uchaguzi ni nzuri

    (GMT+08:00) 2018-07-31 18:46:42

    Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe amesema kuwa anafurahia taarifa nzuri kuhusu uchaguzi uliofanyika jana, ukiwa ni wa kwanza tangu aliyekuwa rais wa nchi hiyo Robert Mugabe kujiuzulu.

    Amesema amefurahishwa na wananchi wengi kujitolea kushiriki kwenye uchaguzi huo, na anasubiri kwa hamu matokeo rasmi kutangazwa kama katiba ya nchi hiyo inavyoelekeza.

    Mshindani wake mkubwa katika nafasi ya urais Nelson Chamasa wa muungano wa MCD pia amesema anatarajia ushindi katika uchaguzi huo.

    Tume ya uchaguzi ya Zimbabwe (ZEC) imesema asilimia 75 ya watu walijitokeza kupiga kura katika uchaguzi huo uliofanyika jana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako