• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Rwanda yajadili utayari wa kujiunga na soko huru la Afrika

    (GMT+08:00) 2018-07-31 19:55:26

    Tume ya Uchumi ya Afrika ECA imesema kuwa bara lote la Afrika litanufaita na mpango wa soko huru barani humo kuliko linavyonufaika na makubaliano mengine ya kibiashara nan chi nyingine.

    Maafisa wa tume hiyo wameyasema hayo wakati wa mkutano wa kujadili sera kuhusu soko huru la Afrika na kutathmini utayari wa Rwanda wa kuingia kwenye soko hilo.

    Taasisi ya sera ya kiuchumi ya Rwanda (EPRN) kwa kushirikiana na tume hiyo ya uchumi na wizara ya biashara nchini humo walishiriki mkutano huo.

    Katibu wa kudumu kwenye wizara ya biashara ya viwanda wa Rwanda Michel Sebera,amesema ili nchi hiyo ijinufaishe na soko huru la Afrika, kwanza inafaa kukuza viwanda na kuongeza ubora kwenye bidhaa zake,

    Makubaliano ya soko huru la pamoja la Afrika yataanza kutekelezwa baada ya kuidhinishwa kwa maazimio 22.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako