• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Amana na mali za benki zaongezeka Tanzania

    (GMT+08:00) 2018-07-31 19:56:01

    Taarifa kutoka taasisi za kifedha nchini Tanzania zinaonyesha kuwa robo ya pili ya mwaka huu (kati ya Aprili -Juni) kumekuwa na ongezeko la amana na mali za benki.

    Taarifa za hesabu za fedha zilizotolewa na benki nyingi zinaonyesha kuongezeka kwa mali na amana za wateja licha ya baadhi kutofanya vizuri.

    Kwa mujibu wa taarifa hizo, mali za Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) ziliongezeka kwa asilimia 6.6 kufikia Sh1.93 trilioni kwenye robo ya pili ya mwaka unaoishia Juni 30, 2018 kutoka Sh1.81 trilioni katika robo ya kwanza inayoishia Machi 31.

    Nazo amana za wateja zimeongezeka kwa asilimia 9.7 kufikia Sh1.37 trilioni kutoka Sh1.25 trilioni kwa kipindi hicho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako