• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Mapato ya Tanzanite yashuka

    (GMT+08:00) 2018-07-31 19:56:19

    Kushuka ghafla kwa mapato yatokanayo na madini ya Tanzanite kutoka Sh444 milioni hadi Sh40 milioni kwa mwezi kumeanza kuwaathiri wakati wa Arusha na Mirerani kutokana na kupungua kwa mzunguko wa fedha, Mwananchi linaripoti.

    Wiki iliyopita mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula na wajumbe wake walitembelea mgodi wa Mirerani na kuwaambia waandishi wa habari kuwa wamebaini utoroshaji wa Tanzanite uliosababisha kushuka mrabaha kutoka Sh444 milioni hadi Sh40 milioni kwa mwezi.

    Alisema wamebaini kuwapo udanganyifu unaofanywa na madalali wanaonunua madini migodini na ambao wamekuwa wakificha madini hayo ili kukwepa ushuru.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako