• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UM waeleza wasiwasi juu ya wakimbizi milioni 1.2 wa ndani nchini Syria

    (GMT+08:00) 2018-08-01 08:51:41

    Umoja wa mataifa umeeleza wasiwasi mkubwa juu ya wakimbizi milioni 1.2 wa ndani nchini Syria katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, na athari zao kwa jamii zinazowapokea. Msemaji mshiriki wa katibu mkuu wa Umoja huo Bibi Eri Kaneko, amesema idadi kubwa ya wakimbizi wa ndani imeweka shinikizo kubwa kwa jamii zinazowapokea kote nchini Syria, na kwamba katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, karibu watu milioni 1.2 wameripotiwa kuwa wakimbizi wa ndani, sawa na wastani wa watu 6,500 kila siku au watu laki mbili kwa mwezi.

    Takwimu pia zinaonesha kuwa wasyria milioni 6.3 wamekimbilia nchi jirani katika miaka saba iliyopita tangu vita ilipoanza nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako