• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki za Kenya zatafakari kuwekeza katika usalama wa mtandaoni ili kutokomeza utapeli

    (GMT+08:00) 2018-08-01 08:52:17

    Benki za Kenya zinapanga kuongeza uwekezaji kwenye usalama wa mtandaoni, ili kutokomeza utapeli wa huduma za fedha kwenye mtandao wa Internet. Ofisa mtendaji mkuu wa Shirikisho la wanabenki la Kenya KBA Bw. Habil Olaka amesema sekta ya benki inaongeza matumizi ya teknolojia ya tehama ili kupanua upatikanaji wa huduma za benki, na vilevile kupunguza gharama za huduma hizo.

    Amesema asilimia kubwa ya matukio ya uhalifu wa mtandaoni yamefanyika kwa kushirikiana na wafanyakazi wa benki, na hivyo wameweka mkazo katika kuwachunguza na kuwafuatilia wafanyakazi wa benki ili kutokomeza uhalifu huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako