• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chama cha ANC chaunga mkono mpango wa kutwaa ardhi bila fidia

    (GMT+08:00) 2018-08-01 09:03:27

    Chama tawala cha Afrika Kusini ANC jana kilitangaza kuwa kinaunga mkono mabadiliko ya kipengele cha 25 cha katiba ya Afrika Kusini, na kusema kinaunga mkono "wazi" kutwaa ardhi bila fidia.

    Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini jana alisema Afrika Kusini inakabiliwa na changamoto nyingi, na hasa swala la kutwaa ardhi. Amesema chama cha ANC kinapongeza wananchi wote waliotoa maoni kuhusiana na suala la ardhi, kwa uwazi na bila upendeleo.

    Amesema mpango wa kutwaa ardhi utawezesha ugawaji wa haki wa ardhi, na kufanya ardhi hiyo itumike kwa maendeleo ya uchumi, kwa kufanya waafrika kusini wengi waweze kutumia ardhi kwa ukamilifu, na kuwezesha ushiriki wa mamilioni ya waafrika kusini kwenye mambo ya uchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako