• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Rwanda yasema uko tayari kuiunga mkono sekta ya nguo bila makubaliano na Marekani

    (GMT+08:00) 2018-08-01 09:03:48

    Serikali ya Rwanda imesema iko tayari kuwaunga mkono wazalishaji wa nguo, baada ya Marekani kufuta makubaliano ya kuingiza bidhaa za nguo nchini humo bila ushuru.

    Waziri wa biashara na viwanda wa Rwanda Bw. Vincent Munyeshaka amewaambia waandishi wa habari nchini Rwanda, kuwa serikali imekutana na wazalishaji na kuwahakikishia kuwa kuna soko kubwa la nguo nchini Rwanda, na wako tayari kuviunga mkono viwanda vya ndani. Lakini pia amewataka wazalishaji hao kuangalia masoko mengine ya Ulaya na Asia, ambako serikali ya Rwanda imesaini makubaliano ya biashara nafuu.

    Waziri huyo amesema hayo kufuatia uamuzi wa Marekani kufuta makubaliano na AGOA kwa bidhaa zote za nguo kutoka nchini Rwanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako