• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda yakaribisha kutolewa upya kwa mamlaka ya tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia

    (GMT+08:00) 2018-08-01 09:16:59

    Jeshi la Uganda limekaribisha kupewa mamlaka upya kwa tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM na kubainisha kuwa hatua hiyo itaisaidia kufikia malengo ya kimkakati.

    Msemaji wa jeshi la Uganda Brigedia Richard Karemire amesema Azimio namba 2431 litawazesha jeshi kutimiza mikakati yake muhimu ya kulinda usalama mchakato wa kisiasa, kusaidia kuwashinda wapiganaji wa kundi la al-Shabab na kujenga uwezo wa majeshi ya Somalia, ili kuchukua majukumu ya usalama wa nchi hiyo.

    Bw. Karemire ameongeza kwamba Maazimio ya Umoja wa Mataifa ni ya lazima kwa nchi za wanachama, hivyo Jeshi la Uganda chini ya AMISOM, litaendelea kufanya kazi chini ya azimio hilo ili kufikia malengo muhimu ya kimkakati ya kuwaunga mkono wasomali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako