• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kundi la waasi la Ethiopia laamua kurudi nyumbani

    (GMT+08:00) 2018-08-01 09:41:17

    Kundi la waasi la Ethiopia, Patriotic Ginbot 7, lenye makao yake nchini Eritrea, limetangaza uamuzi wa kurudi nyumbani, baada ya kufanya mazungumzo na waziri mkuu wa Ethiopia Bw. Abiy Ahmed,.

    Kundi hilo limesema mabadiliko makubwa ya kiuchumi, kijamii na kisiasa yanayoendelea nchini Ethiopia tangu kuapishwa kwa Bw. Ahmed, ni sababu kuu ya uamuzi wao wa kusitisha operesheni za kijeshi, kurudi nyumbani na kushiriki katika kulinda amani na demokrasia ya nchi.

    Mapema mwezi huu, baraza la chini la Bunge la Ethiopia lilipitisha uamuzi wa kuondoa makundi matatu ya waasi, likiwemo Patriotic Ginbot 7, kutoka kwenye orodha ya makundi ya kigaidi ya Ethiopia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako