• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Nigeria achaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa ECOWAS

    (GMT+08:00) 2018-08-01 09:41:58

    Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria amechaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi ECOWAS.

    Rais Buhari amechaguliwa mjini Lome kwenye kikao cha 53 cha Wakuu wa Nchi na Serikali za ECOWAS. Anachukua nafasi hiyo kutoka kwa rais Faue Gnassingbe wa Togo. Uchaguzi wa mwenyekiti, ni moja ya ajenda muhimu za mkutano huo wa kilele wa ECOWAS.

    Kwenye hotuba yake baada ya kuchaguliwa rais Buhari ameahidi kuhudumia na kushirikiana na wenzake kuleta amani, usalama, utawala bora na maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa kanda ya Afrika Magharibi, na kuiendeleza ECOWAS ifikie ngazi ya juu.

    Mkutano ujao wa kilele wa wakuu wa serikali za nchi za ECOWAS utafanyika mjini Abuja tarehe 21, Disemba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako