• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 26 wauawa katika mashambulizi mawili Afghanistan

    (GMT+08:00) 2018-08-01 10:15:02

    Watu 18 wameuawa wakiwemo washambuliaji watatu na wengine 15 wamejeruhiwa katika shambulizi la kigaidi lililotokea jana dhidi ya jengo la ofisi ya serikali mjini Jalalabad, mashariki mwa Afghanistan, muda mfupi baada ya mkutano katika jengo hilo.

    Kati ya waliouawa kuna ofisa mmoja wa polisi na mwanamke mmoja, na majeruhi tisa wameondoka hospitali baada ya matibabu.

    Siku hiyohiyo, watu wanane waliuawa na wengine 40 walijeruhiwa baada ya basi walilokuwa wakisafiria kukanyaga bomu lililotegwa barabarani katika mkoa wa Farah, magharibi mwa Afghanistan, ambao umeshuhudia mapigano makali kati ya vikosi vya usalama na wapiganaji wa kundi la Taliban katika miezi kadhaa iliyopita.

    Hakuna kundi lolote lililotangaza kuwajibika na mashambulizi hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako