• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Timu zaanza maandalizi kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kuu

    (GMT+08:00) 2018-08-01 11:22:52

    MABINGWA wa Afrika Mashariki na Kati, Azam FC imesafiri hadi Uganda kwa ajili ya kuanza kambi rasmi ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, inayotarajiwa kuanza Agosti 22, mwaka huu.

    Timu hiyo ambayo imefanya usajili wa baadhi ya wachezaji ili kujiimarisha imewasili mjini Kampala jana ikiongozwa na Kocha wake Mkuu, Mholanzi Hans van der Pluijm na Msaidizi wake, Juma Mwambusi.

    Nayo timu nyingine ambayo ndiyo mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara kwa msimu uliopita, Simba, inaendelea na kambi yake nchini Uturuki ikiwa ni kwa ajili ya msimu mpya wa ligi unaoanza rasmi Agosti 22.

    Lakini zaidi, timu nyingine shiriki za ligi hiyo zimeendelea kufanya usajili ili kujiimarisha lakini pia zikicheza mechi za kirafiki kama sehemu ya kujiandaa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako