• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • REG na Patriots kucheza mechi ya tatu ya fainali

    (GMT+08:00) 2018-08-01 11:23:16
    Timu za REG na Patriots kesho zinaingia kwenye mechi ya tatu ya fainali ya ligi ya kikapu nchini Rwanda, zikiwa na matokeo ya 1-1 mkononi kutokana na michezo miwili ya awali.

    Katika mechi ya kwanza iliyofanyika Julai 20, Patriots waliwashinda REG kwa alama 63-58, lakini REG walisawazisha matokeo hayo kwenye mechi ya pili iliyofanyika ijumaa iliyopita walipopata ushindi wa alama 73-65.

    Timu itakayoshinda mechi nyingi katika saba zitakazochezwa, ndiyo itatwaa ubingwa wa ligi hiyo, na timu ya Patriots ndiyo mabingwa watetezi wa ligi hiyo baada ya kuwafunga hao hao REG katika mechi za fainali msimu uliopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako