• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kanuni ya adhabu dhidi ya makocha yapitishwa ligi za Uingereza

    (GMT+08:00) 2018-08-01 11:24:15
    Hatimaye Bodi ya ligi za soka nchini Uingereza EFL imepitisha sheria inayowapa mamlaka waamuzi wa mechi kuwaadhibu makocha pamoja na watu wengine kutoka kwenye benchi la ufundi wakati wa mechi.

    Sheria hiyo inamruhusu mwamuzi kutoa kadi ya njano au kadi nyekundu kulingana na vitendo vyovyote ambavyo si vya kiuanamichezo kama ambavyo adhabu hizo hutolewa kwa wachezaji.

    Vitendo ambavyo mwamuzi anaweza kutoka kadi stahili na muafaka kulingana na kosa, ni pamoja na utovu wa nidhamu kwa ujumla, lugha za matusi, matamshi ya kejeli, kupiga teke maji au kitu chochote kwa kuashiria hasira, kwenda eneo la benchi la ufundi la timu pinzani, pamoja vitendo vya kuingia mizozo na mashabiki uwanjani.

    Wingi wa kadi hizo, utazalisha adhabu ya kufungiwa mechi moja au zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako