• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chama tawala nchini Zimbabwe chashinda viti vingi vya ubunge

    (GMT+08:00) 2018-08-01 16:37:46

    Matokeo ya awali yaliyotangazwa jana usiku na Tume ya Uchaguzi ya Zimbabwe (ZEC) yameonyesha kuwa, chama tawala nchini humo ZANU-PF kimeshinda viti 36 vya ubunge kati ya 48 vilivyotangazwa, huku muungano wa vyama vya upinzani nchini humo MDC ukipata viti 11 na chama cha NPF nafasi moja.

    Tume hiyo imesema itaendelea kutangaza matokeo zaidi hii leo kwa kuwa matokeo ya viti 162 kati ya 210 bado hayajatangazwa. Lakini matokeo ya kura ya urais, ambayo rais wa sasa Emmerson Mnangagwa na hasimu wake ambaye ni kiongozi wa muungano wa upinzani wa MDC Nelson Chamisa wanachuana vikali, yatatangazwa mara baada ya kura zote kuhesabiwa nchi nzima.

    Sheria ya uchaguzi nchini Zimbabwe inaelekeza kuwa, matokeo yote ya uchaguzi yanatakiwa kutangazwa kabla ya jumamosi wiki hii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako