• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wapiganaji 200 wa IS wajisalimisha kaskazini mwa Afghanistan

    (GMT+08:00) 2018-08-01 16:42:34

    Gavana wa mkoa wa Jawzjan, kaskazini mwa Afghanistan Bw. Mawlawi Lutfullah Azizi leo amesema, wapiganaji 200 wa kundi la IS wakiwemo baadhi ya viongozi waandamizi wamesalimisha silaha zao katika wilaya ya Darzab mkoani humo.

    Hatua hiyo imekuja baada ya mapambano makali kati ya kundi la Taliban na kundi la IS kwenye wilaya hiyo na eneo jirani la Qush Tepa, ambapo katika wiki tatu zilizopita, wapiganaji 300 wa makundi hayo mawili waliuawa kwenye mapambano hayo.

    Kundi la IS bado halijatoa taarifa kuhusu tukio hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako