• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaweka mipango kuhusu kazi ya uchumi katika nusu ya pili ya mwaka huu

    (GMT+08:00) 2018-08-01 17:10:56

    Mkutano wa Baraza la mashauriano ya kisiasa la China ulioendeshwa na katibu mkuu wa kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China Bw. Xi Jinping, umefanyika mjini Beijing. Mkutano huo umepanga kazi kuhusu uchumi wa China katika nusu ya pili ya mwaka huu.

    kutano huo unaona kuwa, hali ya uchumi imepata mabadiliko katika hatua ya utulivu, na inakabiliwa na changamoto mpya. Naibu mkurugenzi wa Kituo cha usimamizi wa hali ya uchumi cha China kwenye Idara ya takwimu ya China Bw. Pan Jiancheng anasema:

    "Nafuatilia sana makadirio yaliyotolewa kwenye mkutano huo ambayo yanataja kwa mara ya kwanza, kuwa hali ya uchumi ya China imebadilika katika hatua yenye utulivu, na inakabiliwa na changamoto mpya. Mabadiliko hayo makubwa yametokea nje ya China. Ili kukabiliana na mazingira kama hayo, mkutano huo wa Baraza la mashauriano ya kisiasa umeweka mipango halisi."

    Bw. Pan Jiancheng anaona kuwa, mabadiliko ya mazingira ya nje ikiwemo mikwaruzano ya kibiashara kati ya China na Marekani na hali zisizotabirika za mahitaji kutoka nje zinazoongezeka, pamoja na mabadiliko mbalimbali nchini China ikiwa ni pamoja na marekebisho na udhibiti wa mali zisizohamishika, vimewekea shinikizo la kupungua kwa uchumi. Ili kukabiliana na mabadiliko hayo mapya, mkutano huo umetaja bayana kuwa, inapaswa kudumisha maendeleo yenye utulivu na hatua madhubuti ya uchumi, kushikilia kutekeleza sera za fedha za kuchochea uchumi , na kuongeza unyumbufu na ufanisi wa sera.

    Mkutano huo pia umeeleza kuwa, inapaswa kuongeza nguvu katika ujenzi miundo mbinu, uwezo wa kufanya uvumbuzi, kukuza msukumo mpya wa uchumi, na kupunguza gharama za viwanda.

    Katika nusu ya pili ya mwaka huu, China itaadhimisha miaka 40 tangu ianze kutekeleza sera ya mageuzi na ufunguaji mlango. Mkutano huo umesisitiza kuwa, China itaendelea kusukuma mbele mageuzi na ufunguaji mlango, kuendelea kufanya utafiti na kutekeleza hatua muhimu za mageuzi. Mtafiti kutoka Kituo cha utafiti wa maendeleo cha Baraza la serikali la China Bw. Zhang Liqun anasema:

    "Sera ya mageuzi na ufunguaji mlango ni mfumo muhimu wa kuhakikisha maendeleo ya kiwango cha juu. Kutekeleza kwa pande zote hatua za mageuzi, na kupanua ufunguaji mlango, kutahimiza uchumi wa China kupata maendeleo ya kiwango cha juu na pia kutasaidia uchumi wa China kujiunga na mambo ya dunia, na kusukuma mbele mchakato wa mafungamano ya uchumi duniani."

    Kwa mujibu wa mkutano huo, katika nusu ya pili ya mwaka huu, China itatoa kipaumbele katika kudumisha utulivu wa jamii na kuongeza utoaji wa nafasi za ajira. Pia itahakikisha utoaji wa fedha kwa maisha ya watu na kuimarisha kazi ya kuondoa umaskini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako