• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Russia, Irani na Uturuki zasisitiza kuendelea kupambana na Ugaidi na kutafuta suluhisho la mgogoro wa Syria

    (GMT+08:00) 2018-08-01 17:15:17

    Wajumbe wa wawakilishi wa serikali ya Russia, Irani na Uturuki wamekutana huko Sochi, kusini magharibi mwa Russia kujadili masuala kadhaa ya kikanda ikiwemo mgogoro wa Syria.

    Katika taarifa yao, wajumbe hao wamesema wamekubaliana kuendelea kupambana na ugaidi nchini Syria, kutatua mgogoro wa Syria kwa njia ya kisiasa na wameomba kuongezwa zaidi kwa msaada wa kibinadamu na ujenzi wa Syria.

    Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwenye tovuti ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia, wawakilishi wa pande hizo tatu wamekubaliana kuendelea na ushirikiano wa pande tatu kwa makubaliano ya awali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako