• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatakiwa kujenga mfumo wa kuunga mkono unyonyeshaji

    (GMT+08:00) 2018-08-01 18:02:03

    Wiki ya kimataifa ya Unyonyeshaji imeanza leo hadi tarehe 7 mwezi huu.

    Ripoti ya utafiti iliyotolewa hivi karibuni kuhusu vyanzo vinavyoathiri unyonyeshaji nchini China inasema kuwa, ni lazima kujenga mfumo wa kuunga mkono unyonyeshaji nchini humo kwa njia ya kutunga sheria.

    Ripoti hiyo imesema, licha ya kuimarisha zaidi matangazo kuhusu ujuzi na ustadi wa kunyonyesha, na kuinua uelewano wa umma, pia inapaswa kukamilisha utaratibu wa usimamizi wa njia mbadala ya maziwa ya mama, na kutunga kanuni ya usimamizi ya njia hiyo haraka iwezavyo. Pia kukamilisha kutunga sheria kuhusu likizo ya kunyonyesha na bima ya uzazi, kuhakikisha maslahi ya kazi ya mama anayenyonyesha na haki ya mama na mtoto ya kunyonyesha. Vilevile kuunga mkono makampuni kutoa mazingira mazuri kwa wafanyakazi wa kike wanaonyonyesha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako