• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shinikizo la Marekani halitatimiza lengo lake kwa China

    (GMT+08:00) 2018-08-01 19:10:03

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang leo hapa Beijing amesema, shinikizo linalotolewa na Marekani halitafanya kazi, na kama Marekani itachukua hatua zaidi, China nayo itachukua hatua ya kulinda maslahi yake halisi.

    Habari zinasema, Marekani leo itatangaza kuongeza ushuru kwa bidhaa za China zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 200 kutoka asilimia 10 hadi asilimia 25.

    Bw. Geng Shuang amesema, China siku zote inatetea kutatua mgogoro wa kibiashara kati yake na Marekani kwa njia ya mazungumzo, na inasisitiza kuwa ni lazima mazungumzo yafanyike juu ya msingi wa kuheshimiana na usawa, juu ya kuwa na utaratibu na uaminifu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako