• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Madhumuni halisi ya Marekani ya katika mgogoro wa kibiashara kati yake na China

    (GMT+08:00) 2018-08-01 19:53:06

    Hali mpya imetokea katika mgogoro wa kibiashara kati ya China na Marekani uliodumu kwa zaidi ya miezi minne.

    Shirika la habari za uchumi, biashara na masoko la Bloomberg limesema, waziri wa fedha wa Marekani Bw. Steven Mnuchin na mwakilishi aliyetumwa na naibu waziri mkuu wa China Bw. Liu He wanafanya mazungumzo yasiyo rasmi kuhusu kurejesha mazungumzo ya biashara kati ya pande hizo mbili. Wakati huo huo Marekani inapanga kuongeza ushuru kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka China zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 16 kuanzia leo. Ripoti hiyo pia inawanukuu wachambuzi wakisema, serikali ya Marekani inafikiria kuongeza ushuru kwa asilimia 25 kwa bidhaa za China zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 200, ambayo inazidi ile iliyotangazwa ya asilimia 10. Hii inaonesha bayana kuwa Marekani haina moyo wa dhati wa kutatua suala hilo kwa hatua halisi, inachotaka ni kujipatia faida nyingi zaidi kwa njia zisizo halali.

    Tangu Marekani ilipoanza mgogoro wa kibiashara na China Julai 6, watu wametambua kirahisi madhumuni ya serikali ya Marekani ya kufanya hivyo ni kwa ajili ya kuiwekea China shinikizo kubwa zaidi ili kuilazimisha irudi nyuma. Wakati huo huo inataka kugeuza shinikizo kubwa la ndani kutokana na upinzani dhidi ya utozaji wa ushuru kwa bidhaa za China, huku ikitaka kuilazimisha China ifanye mageuzi ya kimuundo kwa kufuata matakwa ya Marekani na kubadilisha njia ya China ya kujiendeleza.

    Lakini kwa kukabiliana na vita vya kibiashara, China haiogopi na hakika itajibu wakati wa lazima, na kama Marekani inataka kutatua suala hilo kwa njia ya mazungumzo inapaswa kuonesha moyo wa dhati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako