• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Singaporea zakubaliana kulinda sera ya pande nyingi na biashara huria

    (GMT+08:00) 2018-08-02 08:03:30

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amsema China inapenda kushirikiana na Singapore kutoa ujumbe wa wazi wa kulinda sera ya pande nyingi na kupambana na sera ya upande mmoja na vitendo vya kujilinda kibiashara.

    Bw. Wang amesema hayo jana alipokutana na mwenzake wa Singapore Bw. Vivian Balakrishnan kabla ya mkutano wa mwaziri wa mambo ya nje wa China na Jumuiya ya Nchi za Kusini Mashariki mwa Asia ASEAN na mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa Mkutano wa Kilele wa Asia Mashariki.

    Bw. Wang amepongeza Singapore kwa kusukuma mbele uhusiano kati ya China na ASEAN kama ni mratibu kati ya pande hizo mbili katika miaka mitatu iliyopita, na kubainisha kuwa China siku zote inahimiza mchakato wa ushirikiano wa kikanda wa Asia Mashariki unaotoa kipaumbele kwa ASEAN. Ameongeza kuwa kutokana na ongezeko la ukosefu wa uhakika na sekta zisizo na utulivu duniani, nchi hizo zinapaswa kufanya juhudi za kivitendo kulinda amani na utulivu wa Asia Mashariki na kudumisha mwelekeo wa kusonga mbele.

    Kwa upande wake, Bw. Vivian amekubali kuwa nchi hizo mbili zinapaswa kujitokeza katika mapambano dhidi ya sera ya upande mmoja na vitendo vya kujilinda kibiashara vinavyoongezeka na kulinda sera ya pande nyingi, biashara huria na mafungamano ya kiuchumi ya kikanda.

    Habari nyingine zinasema siku hiyohiyo, Bw. Wang pia alikutana na mwenzake wa Cambodia Bw. Prak Sokhonn. Mawaziri hao wawili wamekubaliana kuwa nchi zao zitashirikiana kulinda sera ya pande nyingi, kanuni za kimataifa na amani na utulivu wa kikanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako