• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kocha mpya Taifa Stars kuwasili Agosti, amekwishaunda kikosi cha kuivaa Uganda Septemba 8

    (GMT+08:00) 2018-08-02 08:29:00
    Kocha mpya wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) anatarajiwa kuwasili nchini humo mapema mwezi huu kwa ajili ya kusaini mkataba wa kuanza kazi.

    Katibu mkuu wa shirikisho la soka Tanzania (TFF) Wilfred Kidau amesema anaamini kocha huyo atapendwa na watanzania wengi na amekwishaanza kufuatilia wachezaji kwa kushirikiana na benchi la ufundi.

    Baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 nyumbani na Lesotho Juni 10, mwaka jana Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, Taifa Stars itasafiri kuwafuata Uganda kwa mechi ya Septemba 8, mwaka huu kabla ya kuwafuata Cape Verde Oktoba 10 kukamilisha mechi zake za mzunguko wa kwanza kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako