• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanariadha wa Tanzania na Kenya wakwama Nigeria

    (GMT+08:00) 2018-08-02 08:29:27
    Zaidi ya wanariadha 300 wakiwemo wa Tanzania na Kenya na kutoka mataifa mengine ya Afrika wamekwama katika uwanja wa ndege wa Murtala Muhammad 2 mjini Lagos Nigeria.

    Wanariadha hao walitarajiwa kushiriki kwenye mbio za riadha za Afrika zilizoanza jana mjini Asaba, jimbo la Delta, Nigeria.

    Mji huu wa Asaba ulitarajiwa kujizolea sifa kwa kuandaa Makala ya 21 ya riadha barani, lakini kuanzia siku ya jumamosi wiki iliyopita, wanariadha kutoka matafa 52 wamekabiliwa na changamoto za uchukuzi na za usimamizi.

    Wanariadha wa Kenya ndio walioathirika zaidi huku zaidi ya wanariadha 40 wakisalia uwanja wa ndege wenzao wakifanya mazoezi uwanjani wa Lagos.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako