• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IAAF kupambana na ubaguzi wa rangi

    (GMT+08:00) 2018-08-02 08:33:05

    Shirikisho la riadha la kimataifa (IAAF), limeamua kuweka sera ya kupambana na ubaguzi wa rangi kuwa ajenda kuu kwa sasa.

    Hayo yamebainishwa na meneja wa kamati ya tiba ya IAAF, Dk Paolo Emilio Adami, wakati akizungumzia utekeleza wa agizo alilopewa na Mkurugenzi wa IAAF, kuhusu uchunguzi anaopaswa kuufanya kutokana na kukithiri kwa ubaguzi ndani ya mchezo huo.

    Akifafanua hilo, Dk Paolo Emilio Adami amesema wameamua kulifanya hilo wakati huu, baada ya kupokea malalamiko kutoka mashindano ya dunia kwa vijana chini ya miaka 20, yaliyofanyika mwezi uliopita.

    uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa, suala la ubaguzi limeenea katika sehemu kubwa ya Dunia, hivyo uchunguzi wao utapitia mataifa mbali mbali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako