• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uturuki yaapa kulipiza kisasi vikwazo vya Marekani dhidi ya mawaziri wa Uturuki

    (GMT+08:00) 2018-08-02 08:46:56

    Wizara ya mambo ya nje ya Uturuki imesema italipiza kisasi vikwazo vilivyowekwa na Marekani dhidi ya mawaziri wa Uturuki kutokana na kesi ya mhubiri wa Marekani Bw. Andrew Brunson. Taarifa iliyotolewa na wizara hiyo inasema hatua zitachukuliwa mara moja kujibu vikwazo hivyo vya Marekani visivyo na msingi, na pia imelaani wizara ya fedha ya Marekani na kutoa mwito wa kufuta uamuzi wake.

    Mapema jana wizara ya fedha ya Marekani ilisema waziri wa sheria wa Uturuki Bw. Abdulhamit Gul na waziri wa mambo ya ndani Suleyman Soylu wamechukua nafasi za uongozi kwenye mashirika yanayowajibika na kukamatwa kwa mhubiri wa Marekani Bw. Andrew Brunson aliyetuhumiwa kujihusisha na ugaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako