• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Tanzania yawaonya wanaopinga mradi wa bwawa la Stiegler

    (GMT+08:00) 2018-08-02 09:00:13

    Waziri wa nishati wa Tanzania Bw. Medard Kalemani ameonya kuwa serikali itachukua hatua za kumwadhibu mtu yeyote atakayejaribu kuzuia mradi wa umeme kwa nishati ya maji wa Stiegler.

    Bw. Kalemani amesema hayo kwenye mkutano uliowakutanisha mawaziri 11 na makatibu wakuu wa wizara wanaohusika na utekelezaji wa mradi huo. Bw. Kalemani amesema mradi huo unatarajiwa kuzalisha megawati 2,100 za umeme, ambao pia unatarajiwa kutumika kuendesha treni ya umeme, na utakaobaki unatarajiwa kutumika viwandani na majumbani.

    Kwa sasa Tanzania ikiwa na watu milioni 54, ina uwezo wa kuzalisha megawati 1,500 tu za umeme. Mwaka jana serikali ya Tanzania ilitenga dola za kimarekani 307 kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa Stiegler.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako