• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Naibu gavana wa benki kuu ya Afrika Kusini ataka kuwe na maandalizi ya mapinduzi ya nne ya kiviwanda

    (GMT+08:00) 2018-08-02 09:00:36

    Naibu gavana wa benki kuu ya Afrika Kusini Bw Daniel Mminele amesema mapinduzi ya nne ya kiviwanda yanaleta fursa na changamoto, zinazotoa mwito wa kuwepo kwa hatua za makusudi ili kunufaika na mapinduzi hayo.

    Akiongea kwenye chuo Kikuu cha Zululand, Bw Mminele amesema vyuo vikuu na taasisi nyingine za elimu ya juu wana jukumu la kuiandaa nchi kwa ajili ya mapinduzi ya nne ya kiviwanda. Amesema teknolojia mpya zitaleta mageuzi kwenye dunia tunayoishi, lakini kasi na ukubwa wa mageuzi hayo vitakutana na uwezo wenye ukomo na fursa zisizo na ukomo.

    Amesema watunga sera, benki kuu, viongozi wa biashara na mashirika kama BRICS na G20, wanajiandaa kukabiliana na mapinduzi ya nne ya kiviwanda. Amezitahadharisha nchi kuchukua hatua kwani mageuzi yatakuwa ya kasi na hayako mbali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako